TAFUTA HAPA

Cheka uongeze siku za kuishi na story fupi tena nzuri

Ni majira ya saa 11 jioni nikitoka zangu Morogoro kwenye usaili narudi zangu Dar ninapoishi.. Kutokana na ugumu wa maisha, nimebakiwa na shilingi 3000 tu mfukoni hapo nikiwaza chakula cha jioni pamoja na nauli ya daladala..tena ukizingatia Mbagala ilivyo mbali.. Nikajipa moyo siku itapita.

Tulipofika Chalinze, basi lilisimama na akapanda mrembo mmoja matata sana, umri kati ya miaka 24 hadi 26, mwenye urefu wa wastani, mweupe, mwembamba kiasi huku akiwa ametupia suruali ya jinsi pamoja na t shirt iliyomkaa vizuri na kuonesha umbo lake maridhawa la namba nane. Akaja akaketi kwenye siti iliyopo pembeni mwangu kwa kuwa kabla ya kufika chalinze, abiria aliyekuwa amekaa jirani yangu alishuka.. Basi tukasalimiana na safari ikaendelea.

Akajitambulisha anaitwa Karishma.. Na Mimi nikamwambia naitwa Abdulghan nilichukua jina la mdogo wangu abdulghanim ilimradi tu nikaeka zile za kihindi fulani ilimladi mambo yaende sawa. Basi tukapiga stori nyingi sana.. Tulipokaribia kufika Mbezi akaniaga akasema atashuka kituo cha mbezi mwisho kwani ndipo anapoishi. Basi nikamuaga..tukabadilishana namba za simu.. Kwa kweli alikuwa mcheshi sana na nilifurahi mno kupata namba zake nikijua nishapata bint mrembo mwenye asili ya kihindi.. Basi baada ya kufika Ubungo wakati natoa mizigo yangu sehemu ya kuhifadhia, nikaona pochi ya kike.

Nikakumbuka karishma nae aliweka mizigo yake pale..nikasema hebu nifungue niangalie ndani.. Heeeeh nikakuta pesa nyingi sana za kitanzania pamoja na Dola za marekani nyingi sana pamoja na vitambulisho vya karishma. Nikajiuliza, je nimpigie au nipotezee niondoke na pesa?? Wakati nawaza hayo ghafla nikaona simu inaita..Jina ni karishma. Dah..nikawazaaa nikiwazu huku simu inaita..nikaamua tu kupokea,

"Hallo, samahani Abdulghan eti umeona pochi yangu hapo hata sijui nimeipoteza wapi"
Nikamjibu " Yah karishma ndio nimeiona sasa hivi nashuka Ubungo hapa nikawa nataka nikupigie simu"

"Ooooh thanks God! Yaan you can keep hizo hela but please naomba unisubiri nijekuchukua passport na visa yangu  vitambulisho hivyo ni muhimu mno yani"
"Whaaat?? Mbona usiku sana! Are you serious?"
Ilikuwa inakaribia saa 6 usiku.

"Yah, why not? Sawa Nakusubiri Karishma."
"ahsantee akasema Karishma"
"Usijali.. Nikiwa nafijiria sasa akifika usiku huu atarudi kweli kwao ama itakuwaje".
Mawazo yakanijia nitaenda kulala nae kama atakubali.

Dah, ni kama nilichanganyikiwa ghafla.. Nikaona gari aina ya BMW X6 ikiingia langoni Mara nikamuona Karishma akishuka akiwa peke yake.

Nikawa nawaza, sijui itakuwaje huko ndani kama akikubali kwenda kulala na mimi ? Wakati nawaza hayo, mara nasikia Abdulghan nashukuru kwa kunihifadhia vitu vyangu mi siwezi kurudi nyumbani mana nimewaaga nitalala kwa rafiki yangu.


Sasa unaonaje tuende Landmark hotel tukalale pale mpaka asubuhi.
Mimi tena bila ya hiyana nikakubali kinyonge huku nikijua ataingia tu kwenye mtego.

Abdulghan mbona umeitikia kiunyonge au mi stahili kulala na wewe?.
Uzalengo ukanishinda usiseme hivyo Karishma kwanini usistahili?.

Nikapanda kwenye gari mpaka Landmark Hotel tukachukua chumba kimoja nikamuliza Mimi nitalala wapi choon au? Akanijibu utalala kitandani na Mimi.
Hivi naota ama kweli nikasema kimoyoni.
Abdulghan naenda kuoga nawe pia ujiadae nikirudi uende.
Mara akatoka choon akiwa na nightdress hee! Mtoto kajazia nyuma utasema body ya Nissan morano.
Salale! Anakuja kitandani nilipo.

"Unajua nini kilichotoea"
"We Abdulaziz Umejilaza tu hapo kwenye mkeka mbona hao samaki  hivi umeongeza mkaa kweli? Na wakiungua hawo utakula wali na chumvi..."

Dah, mama yangu kaniamsha nilikuwa ndotoni, tena usingizi wa mchana..Duuh!!!
Dah! Hizi ndoto nyengine