TAFUTA HAPA

STORY: NALIA NA NAFSI YANGU (Sehemu Ya Tano) 05

Related image

Sehemu ya:5 

Mtunzi: Agatha Francis

Baraka ambaye ni mume wake hakupendezwa na swali lile aliinuka nakuingia ndani, alipofika ndani alikuta Mark kajiinamia analia, aliumizwa na maneno ya dada yake kiasi kwamba alishindwa kuzuia machozi. Baraka aliumia sana kumuona shemeji yake katika hali ile kwani Mark alikua kijana mpole mstaarabu ambae hakua muongeaji sana.

Alipomuona Mark akasema"shemeji umemuacha na nani Nancy wangu", maana dada anaweza akafanya jambo la ajabu huko nje, Baraka alitikisa kichwa kisha akasema...
"pole sana shemeji yangu, mpenzi wako kaondoka kwani alishindwa vumilia, alipofika hapo Mark aliinuka nakusema kwanini umemruhusu jamani?, nitaiweka wapi sura yangu mimi.

Mwanamke yule kabadilisha tabia zangu leo dada ananifanyia hivi jamani, alilia sana, Baraka aliona hudhuni ya shemeji yake alimkumbatia akimbembeleza anyamaze kwani anaweza jiletea ugonjwa. Mke wa baraka alisikia kelele zile ndani, roho ilimuuma kwani alimpenda kaka yake hivyo akaingia ndani nakusema nisamehe kaka yangu mimi nilikua nakukumbusha tu wazazi walivyosema, huwezi oa mjini, alisema hayo huku sura ikionesha hamaanishi anachosema, haya nyamaza kaka yangu, nyamaza mdogo angu twende kwa mwenyekiti, huyo mama Careen atafika tu huko kwenu ila utaondoka na Suzan alisema hayo huku akiwavutia nje.

Baraka alikua bado kamshikilia shemeji yake Mark kwani Mark bado hakua vizuri, Mark alimuangalia dada yake kisha akasema"nashukuru sana dada yangu kwa upendo wako mimi nitaoa mwanamke ambaye mlimtaka wewe na wazazi ila kamwe siwezi muacha mama Careen", dada alicheka kisha akasema nashukuru umenielewa utajua wewe na wanawake zenu wa mjini matapeli tu mke Suzi bhana na akijua umekuja atafurahi huyo, haya twendeni, alitoka nje nakuawaacha Baraka na shemeji yake. 

Baraka akasema pole sana Mark, Mungu mwema atakusaidia ila kama mama Careen anamapenzi ya kweli kwako kwa hali aliyoiona atakuelewa tu, kwasasa twende kwa mwenyekiti kwanza tukirudi huko tutaongea zaidi sawa shemeji, Mark alishusha pumzi kisha akasema nashukuru shemeji, ila ntamuambia nini mama Careen anielewe mimi jamani, kanifanyia mengi yule mwanamke, hapana shemu maisha yangu nina hakika yatakua magumu.

Usikose sehemu ya 6