TAFUTA HAPA

STORY: NALIA NA NAFSI YANGU (Sehemu Ya Sita) 06

Related image

Sehemu ya:6 

Mtunzi: Agatha Francis 
Kwani naenda ishi namtu sijamzoea kabisa, Alisema maneno hayo huku akilia sana, Baraka alimuhurumia shemeji yake alimfuta machozi nakusema nyamaza Martin, twende kwa mwenyekiti, Mark alifuta machozi na safari ya kwa Mwenyekiti ilianza.

Mke wa Baraka alikua katangulia mbele wao walifuata nyuma, kwakua kwa mwenyekiti hapakua mbali sana basi baada ya muda mfupi tu walikua wamefika, mwenyekiti alikua anatengeneza...
baiskeli yake alipowaona wageni aliwakaribisha vizuri sana, alishangaa kumuona Mark, tena akiwa na hudhuni akasema "Mark umekua sana kijana wangu lakini mbona unaonekana haupo sawa?".

Mark alijilazimsha kucheka kisha akasema kidogo mzee, ila leo sijisikii vizuri, mwenyekiti aliendelea"ooh pole sana umepata dawa lakini"?, Mark alijibu"ndiyo", basi mwenyekiti alimsalimia sana Mark kwani hakumuona kwa muda mrefu, alipomaliza alimuita mjukuu wake wa kiume alitoa jamvi wakaketi, kisha mwenyekiti aliwakaribisha tena na kuwauliza tatizo nini?, dada yake Mark alianza kueleza, ugomvi wao na mzee Mark alieleza kwamba alimkuta mzee huyo akilima shamba lao na alipohoji mzee moto alidai ni shamba lake kitu ambacho si kweli.

Alipomaliza mwenyekiti alisikitika sana nakusema mwanangu poleni sana lile shamba mimi pia na jua ni mali yenu nilipoona mzee Moto analitumia nilidhani mumeelewana, na wewe dada unajua hali yako hiyo usigombane na watu ila kwakua umefika kwangu haina shida, alimuita tena mjukuu wake nakuagiza mzee Moto akaitwe, basi Yule mjukuu wa mwenyekiti alianza safari hiyo na kipindi chote hicho Mark alionekana anamawazo sana.

Baraka alitambua hilo ila hakua na lakufanya. Basi mjukuu wa mwenyekiti alifanikiwa kumkuta mzee Moto, alifikisha ujumbe na mzee Moto alitii wito. Walipofika mzee Moto alishangaa kuona familia ya Baraka pale hivyo alitambua alichoitiwa, Mwenyekiti alisema"karibu mzee Moto nadhani unaelewa kilichokuleta hapa, je unavithibitisho kuhusu mali ile?", mwenyekiti aliuliza. 

Mzee Moto alijibu kwa ukali "sina", ila mali ile ni yangu kwani niliwadai wazazi wao kwahiyo haiwezekani kabisa niache kirahisi, kauli ile ilimfanya mke wa Baraka kucheka, mzee Moto alisema binti unacheka unadhani nachekesha hapa.

Usikose Sehemu Ya 7