TAFUTA HAPA

STORY: NALIA NA NAFSI YANGU (Sehemu Ya Pili) 02

Related image



Sehemu ya:2
Mtunzi: Agatha Francis

 "Sawa mume wangu sasa nimekuelewa sio unakua muoga unadhani tukiacha mali itakuaje ila itakua vizuri sasa ukimpigia simu kaka Mark pia aje maana peke yetu hatutoweza maana tangu aondoke hajarudi kabisa", mke wa Baraka aliongea.

Basi walicheka sana Baraka alimtania mke wake kwakusema mwanamke mbishi wewe ungekua mwanaume sijui ingekuaje usijali lakini Mark nampigia sasa hivi kaniletee...
simu ipo kitandani pale, mkewe aliingia ndani kuchukua simu, alipokua rudi alisema simu yenyewe kuna mtu alipiga sijui nani?,

Baraka alichukua simu kuangalia nani aliyekua amepiga, alishangaa sana kisha akasema ni shemeji Mark, yaani tunamuwaza na yeye anatuwaza wakacheka kisha mke wake akasema piga sasa, Baraka alianza bonyeza simu iliapige mara simu iliita na alikua Mark na mazungumzo yalikua hivi,

Mark:hello

Baraka:habari yako shemeji

Mark:wazima huko jamani

Baraka:sisi wazima sijui huko shemeji

Mark:mimi pia mzima, naomba niongee na dada yangu hapo kama yupo karibu,

Baraka:sawa haina shida, dada yako yupo, alipomaliza alimuewekea simu mkewe masikioni ili aongee na kaka yake

Mke:kaka habari za siku

Mark:nzuri dada, maendeleo?

Mke:salama kaka yangu, mbona kimya kingi jamani, mke wa Baraka alianza kulalamika lakini kaka yake Mark alikatisha mazungumzo yale kwakusema"usijali dada yangu kesho nakuja huko nataka nimlete wifi yako umuone, kwahiyo mapema sana nitakua huko.

mmmh sawa kaka, mke wa Baraka ambaye ni dada wa Mark aliguna, kaka yake alishtushwa kisha aliuliza mbona unaguna dada yangu kuna nini? dada alicheka kisha akasema karibu sana kaka yangu, sisi utatukuta tunawasubiri tu, tutaongea mengi ukifika, sawa kaka alikubali kishingo upande waliagana na simu ilikatwa.

Baraka aliuliza vipi mke wangu anasemaje shemeji yangu maana nimemkumbuka sana, mke wake alijibu"yaani kaka eti anakuja na mwanamke utadhani huku kijijini hakuna wanawake yaani wanawake wa mjini siwapendi kabisa mimi, Baraka alishangaa kisha akasema"lakini mke wangu kwani wanawake wa mjini wana nini?, mbona unamatatizo wewe, wenyewe wamependana ndiyo maana anamleta kwako yaani unagubu kweli wewe kwani wewe kuna mtu alikuchagulia, nini

Endelea kuifuatilia sehemu ya 3