Sikia shem, kilichotokea leo ni makosa mkubwa sana na  tunapaswa kuyajutia,sio kuyarudia kwa makusudi? Alisema James kwa  msisitizo wa hali ya juu, kichwani alikuwa akijiuliza kaka yake alikuwa  wapi wakati shemeji yake huyu anafanya mambo ya hatari namna ile. James  akajaibu kufunga mlango lakini Monica akawahi kuuzuia, ?kweli unaniacha  nikalale na ukame? Kuwa na huruma bwana? alisema Monica kwa sauti ya  kudeka lakini James akajitahidi kuishinda nafsi, maana tayari mnara wake  ulishaanza kutoa huduma lakini uoga ulizizidi hisia za matamanio.  ?nenda kajipoze kwa mumeo aisee, ondoka usije ukaniletea matatizo?  alisema James. ?Paul amelala na amelewa, hawezi kuamka sahivi, mbona  unanifanyia hivyo lakini? alihoji Monica lakini James akajibu kwa  kuufunga mlango kwa kustukiza, akafunga kabisa kwa funguo na kurudi  kitandani, Monica akabaki kaduwaa pale mlangoni, hakuamini kama anaweza  kukataliwa na mwanaume rijali kwa ujio aliomwendea nao James, akaamua  kukubali matokeo na kurudi chumbani kwake ambapo alimkuta mumewe amelala  akikoroma vibaya, akamuangalia kwa hasira sana kisha akaelekea bafuni  ambapo hakwenda kuoga tu bali pia kutuliza mzuka wake kwa njia za asili  ambazo alikuwa akizitumia mara nyingi ashki inapomzidia, kwani mumewe  alimpa haki yake siku ambayo yeye alikuwa na uhitaji, na mara zote zoezi  liliisha pale ambapo mume anakuwa karidhika, hakuwa akijua kama kitendo  kile kina ushiriki wa watu wawili na kila mmoja wao anatakiwa kufurahia  kinachofanyika.
Asubuhi James alichelewa sana kuamka, hii ilitokana na kuchelewa  kulala ambako kulitokana na mawazo mengi juu ya kitendo ambacho  alikifanya na shemeji yake. ?sasa nadhani umeshakuwa mwenyeji, leo  utaenda pekeyako pale kituoni, mimi nitakupitia jioni? Paul alikuwa  akitoa maelezo wakati akimuaga mdogo wake ambaye alionekana bado ana  usingizi. Baada ya kuagana na Paul, James akaelekea bafuni ambapo alioga  haraka akajiandaa kwa kutoka, ?natoka kidogo shem? aliaga James baada  ya kukutana uso kwa uso na shemeji yake ambaye alikuwa ndio sababu ya  kuondoka kwake mapema yote ile, alikuwa anakimbia vitimbwi vyake ambavyo  alijua fika kama angebaki asingeweza kuviepuka. ?mbona mapema hivyo?  Paul si amesema wewe unaenda kzini mchana?? alihoji Monica ambaye macho  yake yalionesha kutojutia hata kidogo jambo walilofanya. ?natakiwa  kwenda mjini kununua baadhi ya vitendea kazi ambavyo sina, pia natakiwa  kupata sehemu tulivu niandae somo la leo? alijribu kujitetea James  ambaye alikuwa hata hawezi kumtazama shemeji yake kutokana na aibu  aliyokuwanayo juu yake. ?we sema hutaki kukaa na mimi tu, hapo mjini  pana umbali gani mpaka upaendee asubuhi yote hii? Ndo kwanza saa tatu,  ngojea kweny saa 6 nitakupeleka? alishauri Monica lakini James  akashikilia msimamo wake na kuondoka.
Akiwa amekaa kwenye bustani fulani nzuri ndani ya jiji akipunga upepo  huku macho yake yakifaidi urembo wa wadada mbalimbali ambao walikuwa  wakija na kutoka katiaka bustani zile, James alikuwa akingojea muda  usogee aelekee kwenye kibarua chake kile ambacho kilikuwa bado kipya  kabisa, nidhamu ya kazi bado ilikuwa ipo kwenye kiwango cha juu kabisa,  hakutaka kuchelewa. Mara simu yake ikaita, akaitoa na kuangalia mpigaji,  akakuta ni Sir Mdharuba, akaipokea na kuanza kuzungumza naye, Sir  Mdharuba akamueleza juu ya mwanamke ambaye alikuwa amekwenda pale  kituoni kuona kama anaweza kupata mwalimu ambaye anaweza akawa  namfundishia binti yake nyumbani, hivyo Sir Mdharuba alitaka kujua kama  James angeweza kuifanya kazi ile ili ajiongezee kipato, James akajibu  kuwa angeweza kuifanya ile kazi na Sir Mdharuba akamtaka kuchukua  usafiri na kufika kituoni haraka sana ili akapatane na mama wa binti  ambaya alipaswa kuwa mwanafunzi wake.
James akafika ofisini na kukutana na mama akiwa na binti yake, binti  huyo alikuwa na mrembo sana, James hakutamani kuyaweka macho yake mbali  na binti yule baada ya kumuangalia. ?huyu ni mwanangu, anaitwa Julieth,  anasoma St. Chritine girls form 5, so tuliuwa tunatafuta mwalimu awe  anakuja kumfundishia nyumbani? alielezea mama yake binti yule mrembo.  ?unasoma Kombi gani dada?? James akauliza kwa sauti ya upole ambayo  ilikuwa na nia ya kumshawishi mama yule kuwa yeye ni kijana mstaarabu.  ?PCM? alijibu Julieth ambaye sauti yake ilifanana sana na muonekano  wake, sauti kama hizi huwa zinatosha kumfanya msichana kuwa mrembo, sasa  Julieth kwake ilikuwa ziada tu, alikuwa ameumbika hasa. ?Okay so  ulikuwa unataka kusoma masomo yote matatu au?? aliuliza James. ?hapana,  nataka kusoma PURE tu, am not good in it at all? alisema Julieth  akimaanisha anataka kusoma somo la hesabu,somo ambalo mara nyingi huwa  ugonjwa kwa wadada hasa wadada warembo. ?okay, tutasoma ila nataka ufute  kwanza wazo la kwamba Maths ni ngumu, hukupata tu waalimu wazuri, sasa  umepata mwalimu na tatizo limeisha? alisema James kwa utani na wote  wakacheka. Baada ya kubadilishana namba za simu James akawatoa wageni  wake mpaka ambapo ilikuwa imepaki gari yao. ?unaweza kuondoka tu na  gari, mimi dereva wa ofisini atanichukua pale kwenye mgahawa? alisema  mama Julieth kumwambia mwanae, ?lakini please go home, usipitie pengine  popote? aliongezea akimkabidhi mwanae funguo, akaondoa gari ile huku  akiwaacha James na mama yake kila mtu akichukua njia yake.
James alijikuta amempenda sana binti yule lakini alijiona kama hakuwa  na nafasi mbele yake maana alionekana waziwazi kuwa mtoto wa ushuani,  hawa huwa wanaenda na waishua wenzao, sio mtoka kijijini kama mimi,  aliwaza James ambaye alikwenda ofisini kupiga story na Sir Mdharuba  akingojea muda wa kipindi chake ufike, ?haya sasa nimekupa pasi safi  kabisa, akushinde mwenyewe mtoto mzuri yule? alitania Sir Mdharuba  ambaye alionekana kuwa mtu wa totoz sana, James akacheka tu na kubadili  mada.
Baada ya kumaliza kipindi James akatoka na kumpigia Julieth kutaka  maelekezo zaidi ya kufika kwao, kama ambavyo walikuwa wamekubaliana.  ?kwani wewe uko wapi?? aliuliza Julieth baada ya James kumwelezea lengo  la kumpigia. ?mimi ndo natoka ofisini? alijibu kwa kifupi James, basi  Julieth akamuelekeza kwenye mgahawa ambao ulikuwa karibu akimtaka  amsubiri hapo akamchukue. Baada ya dakika kama kumi Julieth akawa  amefika, na akashangaa kumuona James akiwa amesimama nje ya Mgahawa ule,  akshusha kioocha gari na kumuita, safari hii alikuwa amekuja na gari  tofauti na ile ya mwanzo. ?mbona umesimama nje sasa?? si ungeingia  ukapumzika?? alihoji Julieth akiondoa gari baada ya James kuingia. ?aah!  Hii migahawa yenu haiaminiki, unaweza ukanywa juice tu wakakudai elfu  20, nikaona nikungoje nje nisije nikavuliwa shati bure? alisema James na  Julieth akacheka sana. ?jamani, nilikuwa nakuja kulipia chochote  ambacho ungetumia? alisema Julieth ndani ya kicheko. ?ndo ungejieleza  vizuri sasa, mi nimeogopa bwana?.
Safari yao ikkomea kwenye jumba moja la kifahari maeneo ya ushuani,  Julieth akapiga honi, geti likafunguiwa na mtu ambaye bila shaka alikuwa  na mlinzi kutokana na sare alizokuwa amevaa. James akaongozana na  Julieth kuelekea ndani ya jumba lile ambalo James huonaga kwenye TV tu  majumba ya aina ile. James akakaibishwa vizuri, akapewa na Juice kisha  wakapumzika kwa kama dakika 20 kabla ya kazi ya kufundishana kuanza.  Julieth hakuwa kilaza kama ambavyo James alimdhania mwanzo, alionekana  kuwa na kichwa kizuri sana ila hakuwa na mapenzi na somo lenyewe, James  aliligundua hilo mara moja na kuamua kufundisha katika hali ya kutaniana  sana na kuuhusu Julieth amzoee ila baadae ampende, maana aliamini kuwa  ukimpenda mwalimu lazima ulipende somo lake na hiyo ingekuwa dawa tosha  kwa Julith.
?kwakweli siamini, logic imenitesa sana hii huko shule, kumbe ni  rahisi hivi?? alisema Julieth wakati akimtoa James baada ya kumaliza  kipindi. ?mwalimu wako hakujua namna ya kukufundisha, nakuhkikishia  hakuna hesabu ngumu, ukiniamini katika hilo basi umepona? alisema James  kisha wakaagana, Julieth alionekana mwenye furaha sana, tabasamu  halikuisha usoni kwake, James alitamani kuendelea kumuangalia tu lakini  ndo hakukuwa na sababu ya kubaki pale ili aendelee kumuangalia kwani  kipindi kilikuwa kimeisha kwa siku hiyo.
James alifika nyumbani majira ya saa 2 usiku, akamkuta Monica  nyumbani akiwa pekeyake, cha ahabu siku hiyo Monica aionekana kumnunia,  alikuwa tofauti sana na jinsi alivyomuacha asubuhi. James akampa salam  ambayo aliijibu kama hataki, James akaamua kumpuuza na kuingia chumbani  kwani hakuona kama alifanya kosa kukataa ujinga wake.
Alipofika chumbani katoa simu yake ambayo hakuwa amejishughulisha  anyo kwa muda mrefu sana, alipoingalia akagundua kulikuwa na sms 4,  akazifungua na kugundua 3 zilikuwa za Monica na moja ilikuwa ya Julieth,  akaanza na ile ya Julieth ambayo ilikuwa imeandikwa ?nimekupenda sana  Teache James, wewe unajua namna ya kunifundisha, natamani ungenifundisha  na vitu vingine?, James akashangazwa sana na ujumbe ule, akajiuliza  kama kweli ulikuwa ukimanisha ambacho alikuwa anakifikiria au ulikuwa na  maana nyingine ?atakuwa anataka kuongeza somo huyu, labda anataka  nimfundishe na Physics au Chemistry? aliwaza James huku akiijibu sms ile  ?usiwe na shaka, ni wewe tu niko vizuri pia kwenye Physics na  Chemistry?, kisha akafungua sms za Monica, moja iliandikwa ?mambo? Uko  wapi?’ nyingine ilisomeka ?uwahi kurudi tuje kuendelea na darasa letu,  unajua hujakamilika kama mwanaume kama hujui mabo yetu yale? nyingine  ilisomeka ?mbona hujibu sms zangu? hapa ndipo akagundua kwanini Monica  amenuna, alifikiri kuwa sms zake hazikujibiwa makusudi. Wakati  akiendelea kulitafakari hili mara sms ikaingia, ilikuwa inatoka kwa  Julieth ?mimi sina tatizo lolote kwenye Physics wala Chemistry, wala  sihitaji msaada wako upande huo?, sms ile ikamuacha James njia panda,  akabaki akijiuliza kitu gani anataka mtoto huyu? Au fikra zangu za awali  zilikuwa sahihi? ?sasa unataka nikufundishe nini kingine?’? akauliza  kwa sms James baada ya yeye kutokuwa na majibu ya uhakika, akabaki  kaikodolea macho simu yake akingojea kwa hamu jibu la Julieth, ?mapenzi?  Julieth akajibu kaujumbe kafupi tu, lakini kalitosha kuikologa akili ya  James, akabaki akijiuliza anachokiona kweli au ndoto, akiwa kaikati ya  mawazo ujumbe mwingine ukaingia ?sio siri nimekupenda na nataka uwe  wangu ila sijui chochote kwenye mapnzi, nategemea uwe mwalimu wangu?,  James hakuamini anachokiona, ni kweli alimpenda sana Julieth ila  hakudhani anaweza naye anaweza kumtaka mtu kama yeye,sasa nitamfundisha  nini ikiwa mimi mwenyewe sina nijualo? Alijiuliza James, mwisho  akachukua simu yake na kutuma ujumbe ?samahani, nikiwa kazini sishiki  simu, ila niko tayari kwa darasa? kabla hajaituma akajiuliza mara  mbilimbili kama aitume sms ile ama laa, mwisho akafumba macho na  kubonyeza kitufe cha kutuma. Baada ya sekunde chache ujumbe wake  ukajibiwa ?kama unataka kujifunza nitakufundisha ila kwa mashariti  matatu? James akajaribu kutabiri hayo mashariti lakini akafeli mwisho  akaamua kutuma tena ujumbe ?masharti gani tena hayo?
****************************************
 ……………………………………Usikose sehemu ya 4