TAFUTA HAPA

RIWAYA: SHEMEJI MONICA – Sehemu Ya Sita

Pale ndani James alishaanza kuchanganyikiwa, maneno ya mama Julieth yake yalionesha kuwa alikuwa na mashaka ya nini kinafanyika nyani, hasa baada ya kuona mlango umefungwa, ?tuko busy? alijibu Julieth kwa sauti ya juu. ?njooni basi angalau mpate chakula kwanza, muda umeenda? alisema mama Julieth na kusababisha James kuangalia saa yake na kugundua kuwa ilikuwa saa mbili na nusu usiku. ?tunamalizia? alijibu Julieth na mama yake akaondoka. ?inabidi niondoke, tutawaudhi wazazi sasa? alisema James huku akisimama, Julieth naye akasimama na kumpiga busu zito mdomoni, kisha akatangulia kufungua mlango James akifuata nyuma yake. ?karibu tujumuike mezani mwalimu? alisema baba yake Julieth ambaye alikuwa kwenye safari ya kutoka eneo la kupumzikia pale sebuleni, kuelekea eneo la chakula. ?asante mzee muda umeenda sana, nitakula siku nyingine? alijibu James kwa kifupi akiendelea na safari yake ya kwenda nje. ?kwa heshima yangu naomba tupate mlo wa pamoja leo? alisema baba yake Julieth, maneno ambayo James hakuwa na nguvu ya kuyapinga. Wakajumuika mezani na kupata chakula, chakula kilikuwa kitamu kikitawaliwa na mazungumzo ya hapa na pale, baba yake Julieth alikuwa mcheshi sana na alikuwa hakauki simulizi z kuchekesha, hivyo muda wote wa chakula walikuwa wakicheka kwa furaha. James aligundua Julieth ambaye walikuwa wamekaa kwenye meza wakitazamana alikuwa akitumia mudamwingi kuuangalia zaidi ya kula na macho yao yalipogongana alitabasamu, ikambidi James kujitahidi kumkwepa kwani alidhani wazazi wa Julieth wangeweza kusoma jambo pale. Baada ya chakula hakuna ambaye alikuwa na sababu nzuri ya kumzuia James asiondoke, japo mama yake Julieth alimtaka kumpa namba zake za simu ili iweze kurahisisha mawasilano kama angemuhitaji, jambo ambalo James alilitekeleza bila wasiwasi wowote.
Alipofika nyumbani James alishangaa kumkuta kaka yake, ilikuwa ni mapema mno kwa kaka yake kuwepo nyumbani, maana toka alipofika kwenye mji ule kaka yake alikuwa akichelewa sana kurudi nyumbani na hurudi akiwa amelewa, lakini siku hii hakuonekana kama aliyelewa. ?naona umekuwa mwenyeji sana sasa? alisema kaka yake James huku akitabasamu. ?yeah, sasa mtu haweza kunipoteza mji huu? alijibu James, wakacheka. ?sasa wameanza hata kuniibia mume, dalili mbaya hizi za kurudi mida hii? alitania Monica. ?pengine mume anakuwa nje anakutafutia, acha wivu? alijibu kaka yake James ambaye dongo lile la mkewe japo lilikuwa utani lakini linnamlenga yeye zaidi. ?shemeji karibu chakula? alisema Monica akimuelekeza James kuelekea mezani kupata chakula, hali ya meza ilionesha kuwa wengine wote walikuwa wamekula tayari. ?asante shem, ila nimeshakula tayari huko nitokako? alijibu James. ?jamani jamani dalili mbaya hizi? alitania tena Monica, wote wakacheka. ?shikamoo bamdogo? alisalimia Peter, mtoto wa Paul ambaye alikuwa akitokea chumbani, Peter alikuwa amekuja siku hiyo kutokea shule ambako alikuwa akisma ‘boarding’. James akafurahi sana kumuona mtoto huyu wa kaka yake ambaye hakuwa ameonana naye kwa kipindi kirefu, wakasalimiana na kuulizana maendeleo ya shule. ?hii ni suprise kwelikweli, sikujua kama kinaja anakuja leo? alisema James. ?we huoni leo baba yake mapemaaa yuko nyumbani, kama sio ujio wa mwanae angekuwa hapa saa hizi?? alilenga dongo lingine Monica ingawa alilitoa kama anatania. James hakupenda hali ile ya Monica kuwa anamrushia mume wake vimaneno, alijiona kama alikuwa na mchango mkubwa kwenye kusababisha Monica afanye vile kutokana na mambo ambayo wamekuwa wakiyafanya, pengine yamepelekea kumuona mume wake hana maana yoyote,pamoja na kuwa asilimia kubwa ya matatizo yale aliyasababisha yeye mwenyewe (kaka yake James). James akajikuta amepata wazo la ghafla, akaona kuendelea kuwepo mule ndani kunaweza kusababisha mpsuko siku moja, hasa kutokana na mambo ambayo amekuwa akiyafanya na shemeji yake, akaona utatuzi ni kuhama mule ndani. ?jamani mimi nilikuwa nawaza kupanga chumba nianze kujifunza maisha? alijaribu kuliingiza wazo lake kwenye vichwa vya wenyeji wake hawa ili kuona litapokelewaje. ?kwanini umefikia uamuzi huo, kuna jambo lolote limekukera?? alihoji kaka yake ambaye habari hizi zilikuwa za ghafla sana kwake, hakutegemea kuona mdogo wake huyu akiondoka kwake hivi karibuni. ?hapana, nimeishi kwa amani sana ndani ya nyumba hii, na ninashukuru sana ila nadhani ni wakati wa mimi kujaribu kuwa mkomavu na kujitegemea? alielezea vuzuri James na kaka yake akamuelewa haraka. ?au kwasababu Peter karudi umeona chumba hakiwatoshi?? alichangia Monica. ?kwani Peter ni tembo? Chumba chote kile kinaachaje kututosha?? alijibu James kiutani na wote wakacheka. ?lakini huna muda mrefu utaenda chuo, sasa huoni kama hiko chumba hata hutokikaa?? alihoji tena Monica ambaye James alitarajia upinzani mkali kutoka kwake. ?maamuzi yangu ni kutokwenda tena kijijini, maisha yangu yatakuwa hapa, hata kama nitakuwa nakwenda chuo likizo zote nitakuwa hapa kwahiyo chumba changu kitatumika tu? alijibu James. ?mi nadhani sio jambo baya, maadam umeamua mwenyewe na unaamini kuwa utamudu changamoto za maisha, bora tukutakie kila lakheri? alisema kaka yake James na Monica akaonesha kukubaliana, jambo ambalo James hakulitegemea. Wakaendelea na story za hapa na pale mpaka walipochoka na kwenda kulala.
?Aisee Sir Mdharuba natafuta chumba bwana, sijui nitapata wapi?? alianziasha maongezi James wakiwa ofisini akingojea muda wa kipindi chake ufike. ?Vyumba vipo tu humu mjini, unataka cha aina gani kwani?? alisema Sir Mdharuba na kuunganishia na swali. ?cha kawaida tu, cha bei poa? alijibu James. ?hivyo vinapatikana uswahilini, hata pale ninapokaa mimi kuna chumba kiko wazi, kama vipi ukapaone kama panakufaa?. ?sasa si kesho tena hiyo maana naona kama leo muda umeshaenda? alijibu James. ?tunao muda, kwani una dakika ngapi kabla ya kipindi?? alihoji Mdharuba akiangalia saa yake. ?kama 25 hivi? alijibu James mara baada ya yeye kuangalia saa yake pia. Mdharuba akaona zinaatosha sana, wakaondoka pale kituoni kwa kutumia pikipiki ya Mdharuba mpaka maeneo ya uswahilini ambapo alipelekwa kwenye nyumba kubwa yenye vyumba vingivingi kila kimoja kikijitegemea, ilikuwa imejengwa maalumu kwaajili ya kupangisha. James akaoneshwa chumba ambacho kilikuwa tupu, akakiangalia na kuona kilikuwa kinamfaa, akakutanishwa na mma mwenye nyumba ambaye alimpa masharti ya nyumba akaridhikanayo na kulipia pesa ya miezi 6 kama ambavyo mama mwenye nyumba alitaka. Bei ya chumba ilikuwa elfu 20, hivyo kwa miezi 6 ilikuwa ni laki moja na elfu 20, gharama ambayo James aliimudu.
Wakiwa wamerudi kituoni na James akawa anajiandaa kwenda kuanza kipindi chake, simu yake ikaita, namba ilikuwa ni ngeni kwenye simu yake, hivyo hakujua nani alikuwa anapiga, ikambidi kupokea ili kujua mpigaji alikuwa nani. ?hallo James tunaweza kuonana kwenye mgahawa wa hapa nje ya ofisi yenu?? James hakuhitaji kuambiwa kuwa ile ilikuwa ni sauti ya mama yake Julieth. James hakuweza kukataa wito ule, akawaomba wanafunzi wake kumvumilia kwa dakika chache kisha akaenda kumsikiliza mama yake Julieth huku akiwa na wasiwasi mwingi wa juu ya jambo ambalo alitaka kuongelea.
?shikamoo mama? alisalimia James wakati akivuta kiti na kukaa akitazamana na mama yake Julieth. Baada ya kuitikia salam mama Julieth akaanza kuelezea juu ya ujio wake. ?James nataka uniambie ukweli nini kinaendelea kati yako wewe na Julieth? alihoji mama yule, sauti yake ilionesha kuwa alikuwa serious sana na ambacho alikuwa anakifanya. ?sijakuelewa swali lako mama, mblai na kumfundisha Julieth nini kingine kinaweza kuwa kinaendelea?? James alijifanya kama hakuwa na ambalo analijua. ?Julieth ni mwanangu, namjua vizuri sana, hawezi kuficha hisia zake mbele yangu. Jana wakati wa chakula nimegundua kuwa Julieth anakupenda, unaweza kubisha??, mama Julieth akaanza kutumbua jipu na kumuacha James njia panda. ?mama mimi ninachofanya ni kumfundisha Julieth, sina jingine. Siwezi kubisha juu ya kuwa ananipenda maana sijui kilichomo moyoni mwake, illa hajawahi kuniambia na kuna mpaka mkubwa kati yetu, hatuendi zaidi ya kwenye masomo? alijibu James. ?basi wacha nikuulize swali la mwisho na naomba unijibu ukweli? alisema mama Julieth na James akawa tayari kupokea swali hilo. ?tukiachana na swala la kuwa na uhusiano ama kutokuwanao je, unampenda Julieth??. Swali hili lilikuwa gumu sana kwa James kusema kuwa hampendi Julieth mbele ya mama yake ilhali alikuwa akimpenda sana aliona kama ni usaliti, na akajikuta kutmani kusema ukweli.
****************************************
……………………………………Usikose sehemu ya 7