So watu hutongoza vipi?
Hivi kuna kanuni zozote za  kutongoza? Je kuna sheria flani ambazo watu hufuata ambazo hutumika? Ama  huwa inakuja tu yenyewe wakati wa kutongoza? Kwa wanawake, kutongoza si  jambo la lazima, kwa sababu kuna asilimia kubwa ya mwanaume ambao  huanzisha kutongoza. Lakini wakati mwingine inatokea kuwa mwanamke  anapaswa kuchukua hatua ya kuanza kumtongoza mwanaume.
 Wakati ambapo mwanamke anahisi ya kuwa hapati atenshen  inayotakikana, anaweza kuamua kuchukua hatua nzito ambayo inaweza  kufanya kazi ama kutoweza, kwa lengo moja la kuhakikisha kuwa anaonekana  na mwanaume. Mara nyingi hatua hizi huwa zinatokana na maonyesho ya  runinga au filamu.Ok. kuna njia kadha wa kadha ambazo mwanamke hutumia kumtongoza mwanaume. Zile ambazo hujulikana sana ni kama:
- kuangalia macho
- kumnunulia mwanaume kinywaji
- kumsifu
- kutabasamu
- nk
Hii ni baadhi ya kutongoza  ambakwo mara nyingi hufanya kazi. Lakini kuna baadhi ya wanawake ambao  hawaridhiki na hatua hizi na hujaribu kutafuta mbinu nyingine ambazo  wanaamini ya kuwa zinaweza kumsahiwishi na kumtia box mwanaume, baadhi  ya mbinu hizi huwa sawa na nyingine huwa potoshi.
Je ni mbinu gani za kutongoza ambazo wanaume huchukizwa?
Mbinu hizi awali zilikuwa  zikitumika kwa njia rahisi sana lakini kwa sasa zimepitwa na wakati na  huashiria mambo tofauti. Ushauri kwa mwanamke ni kuwa kama iwapo unataka  mahusiano ya kufaana na mwanamke basi usiwahi kutumia kamwe hatua hizi.
1. Kuyapanga matiti yako
Hii inakubalika kutumika kama  ni dharura. Kawaida hakukosekani sehemu ya mapumziko ya mwanamke iwapo  anataka kuyatandaza ama kuyatengeneza matiti yake.
Kuyatengeneza matiti yako yakae  vizuri hadharani inaonyesha kukosa ustaarabu na kukosa heshima kijamii.  Si hivyo pekee bali pia wanaume hawavutiwi kamwe na hatua kama hii.  Ukianza kuyatandaza matiti yako huku na kule kunawafanya wanaume  kujihisi kuwa na aibu kimpango. 
2. Kuramba midomo yako kiushawishi
Kuramba midomo yako kwa njia ya  kuifanya iingiwe na unyevu inakubalika. Lakini kuramba midomo yako kana  kwamba mwanaume ulietoka naye deti ni ice cream ambayo unataka kuila  inaogofya. Mwanzo kwa mwanamke ukiwa unaramba midomo yako kwa ushawishi  kunaweza kumfanya aongope kuwa unaweza kumla wakati ambapo mtakuwa  wawili pekeenu. Ok, najua kuramba midomo huwa kunaleta hisia za mapenzi  lakini haipaswi kufanywa hivyo sehemu za hadhira.
3. Kuomba msaada wakati ambapo hauhitajiki
Kuna tabia ambayo wanawake  hupenda kuitumia mara kwa mara, tabia ya kufanya kitu kuwa kina dharura  na ambacho anahitaji msaada wa haraka kutoka kwa mwanaume. Jambo la  rahisi analifanya kuonekana zito.
Wanaume wanapenda wanawake  ambao wanapenda kujitegemea wao wenyewe, na ambao hawaonyeshi pupa ya  kutaka usaidizi hata kama wanataka.
4. Kurusha nywele kupindukia
Mwanamke anapaswa kuzirusha  nywele zake nyuma wakati ambapo anamtongoza mwanaume lakini haufai  kuzidisha. Kila kitu kina kiasi flani. Hivyo kabla kuzirusha nywele zako  mara kwa mara hakikisha ya kuwa hazitorusha chembechembe yeyote za  uchafu ama kutoa harufu ambayo inaashiria hazijaoshwa kwa muda.
5. Michezo ya kumfinya, kumgonga, kumpiga kofi nk
Je wewe huona kuwa kufanya  hivyo ni furaha? Kwa mwanaume ni LA, ni vile tu hawapendi kusema kwa  nguvu. Lakini ukweli ni kuwa wanaume hawapendi kuumizwa na kugongwa  haswa sehemu za hadharani. Uchungu ni ule ule hata hauchagui unamuumiza  nani. Hivyo tabia kama hiyo haiwapendezi kamwe wanaume.
6. Kujishika kope zako
Huwa inaonekana vizuri wakati  ambapo unafikiria jambo kama hili, lakini wanaume wanapoteza umakini wao  kwa mwanamke iwapo kila mara atakuwa akizishika kope zake. Hii ni mbinu  ya kutumiwa mara moja na wala si kila wakati. Mara nyingi itaoneka  kwamba kuna kitu kimekuingia machoni mwako, na mwanaume hawezi kujizuia  ila kujaribu kukupuliza ili kusaidia kutoa huo uchafu. Mara nyingi hatua  hii inafanya mwanaume apoteze umakini kwako kwa sababu ya hilo jambo.
7. Kuandama wanaume kila mahali
Wewe umekuwa mtu mkubwa hivyo  tabia za kufuata na kuandama watu kila mahali si mpango. Unafaa kuacha  kuandamana na wanaume kila mahali na uanze kuzungumza kile ambacho kiko  alikini mwako. Fahamu ya kuwa tabia ya kuandamana mtu kila mahali huwezi  kutofautisha iwapo umependezwa ama una tabia za kunyatia.
8. Kula chakula kutoka kwa sahani ya mwanaume
Hii ni tabia ambayo kuna  wanawake ambao wanaipenda sana. Mbona usingojee kama mwanaume ataagiza  kula kwa sahani yake? Kawaida kuna kitu ambacho hakitaonekana sawa iwapo  utarukia kuanza kula katika sahani ya mwanaume. Kama umekuwa ukideti na  mwanaume kwa muda mrefu hio ni sawa. Lakini iwapo umeanza kujuana na  mtu hivi karibuni na kuanza tabia kama hii humchukiza mwanaume hapo  hapo.
9. Kujaribu kuongea kuhusu vitu mwanaume anapenda halafu kushindwa kustahimili
Wanaume wengi huona ya kuwa  inakaa raha iwapo kuna maslahi ambayo anagawa sawa na mwanamke. Lakini  iwapo mwanamke ataiga na kujifanya ya kuwa anagawa interest moja na  mwanaume huwa kawaida atagundulika. Mwanaume anapenda uulize na kujua  vitu anavyopenda. Hawataki uanze kutoa ujuzi na ujanja wote kuhusu jambo  fulani bila wewe mwenyewe kujua chochote ambacho unaongea.
10. Kulalamika kihatia
Wanawake kulalamika kihatia  huwa ni jambo zuri la kuweza kuteka atenshen kutoka kwa mwanaume, lakini  kwa mwanaume anajua hio ni mbinu ambayo mwanamke anaitumia kama mchezo  wa kuichanganya akili yake, Hata kama ulikuwa unataka atenshen ndogo  kutoka kwake, mwanaume ataona kwamba umefanya hivyo maksudi kwa ajili  yao, So tabia kama hio inaweza kuharibu siku yao, na pia wewe iwapo  hawaingiliana na ujanja wako.
Hivyo kama kweli unamtaka  mwanamke, tungekushauri uwe mkweli na mwenye mwelekeo. Kama mwanaume  hakuvutiwa kwako, ni vizuri uchunguze chanzo chake badala ya wewe  kujaribu kutongoza kwa njia ambayo inaenda mrama.