Unapohusiana na mtu kimapenzi unafanya naye agano la damu. Agano hilo  maana yake ni kwamba wewe unakubaliana na kufungamana na sifa na tabia  pamoja na vifungo vingine vyote kama vile laana, mizimu, matatizo na  majanga mbalimbali yanayomhusu huyo uliyefanya naye mapenzi, kadhalika  na yeye anafungamana na wewe katika mambo hayo. Agano la namna hiyo  humtaka aliyeingia katika hayo mapatano kukubaliana nayo “consistently”.  Iwapo mhusika hatatii au ataenda kinyume na agano, ndipo agano hilo  “hutrigger malice” na kusababisha kutokuelewana, vurumai, kutokupendana  na hata kuuana katika mahusiano na mara nyingi kupelekea kuachana!
Kimsingi, unapojamiana na mtu unakubaliana naye kuchangia kila  kilicho chake, na yeye pia anakubaliana kuchangia na wewe kila kilicho  chako, hasa laana na matatizo kama vile magonjwa na mizimu kwa sababu  hivi vitu vimejengwa katika maagano ya damu.
Ndio maana wakati mnaoana na mwenzio mlipendana sana, lakini kwa  sababu wewe au mwenzi wako alichepuka na kufanya maagano: ugomvi,  mapigano, kutishiana, chuki na hata kutaka kuuana hakuishi kila leo!  Swala sio wivu kwamba unahisi mwenzi wako anakusaliti au kuhitilafiana  katika mambo tu ya kawaida, issue ni yale maagano ya damu ambayo  “hudemand price”!
Mara nyingi unasikia watu wanalalamika kuhusu tabia za watoto “huyu  mtoto tabia kaichukua wapi, mbona baba na mama yake au ukoo wao hawako  hivyo?”. Chanzo cha tabia za ajabuajabu za watoto ni matokeo ya  michepuko iliyofanya maagano na watu/koo zingine zenye laana. Laana na  matatizo yanayoletwa na agano la damu katika familia havihitaji mtu  kuchepuka na kuzaa nje ya ndoa, bali tu kuhusiana katika mapenzi!
Mimi nilipoingia kwenye mahusiano na mke wangu nilivunja maagano yote  kwa jina la Yesu. Lakini kumbuka kuwa huwezi kuvunja maagano kama vile  ya michepuko kwa jina la Yesu ili “kufavor your own evil deeds”!
Maagano yanayofanywa na watu kwa njia ya mapenzi huenda vizazi hadi  vizazi. Hii ni sawa kabisa kwa mjibu wa sayansi kwani “hereditary  information” kutoka kizazi hadi kizazi hubebwa na viasili vilivyopo  katika damu, mfano DNA.
Pasco anaweza kuendeleza hii mada kwa uchambuzi zaidi.
Mie na mke wangu tuna furaha fulltime kwa sababu mapenzi yetu  yananawiri kila kukicha, na huwa hatuelewi kabisa matatizo katika ndoa  za watu yanatokana na nini! “We are the happiest couple” kwa sababu “we  posses several life secrets” mojawapo ni siri kuhusu agano la damu!
        
Tambueni ya kwamba one of the great decisions a person can make in  his/her life ni kuwa na uhusiano wa kimapenzi (hata kwa dakika moja) na  mtu kwa sababu anafanya naye life covenant “blood covenant”!
We teach you things that matter most!