JAMANI MIE UKAHABA SASA BASI" PART 1
AMANI MIE UKAHABA SASA BASI ni Hadithi inayomuhusu  binti wa kitanzania alietunukiwa uzuri wa asili na mvuto wa kipekee  aliojaaliwa na mungu ama hakika uzuri aliokuwa nao ulikuwa ni kishawishi  tosha kwa mwanaume yoyote aliemtazama binti huyu na kutamani kuwa nae  kutokana na mvuto aliokuwa nao binti huyu anaitwa Jenifer na amezaliwa  katika familia duni ya Mr. Brown na Mrs. Brown yenye watoto watatu (3).  Ambao ni Peter, Joseph na Jenifer na katika watoto hawa watatu mwanamke  alikua ni Jenifer peke yake na ndie alikua mtoto wa kwanza kuzaliwa  katika familia hii yenye watoto watatu ambapo Peter na Joseph walikua ni  wadogo zake na Jenifer na walikuwa bado ni wadogo sana. Na wazazi wa  Jenifer Mr. Brown na Mrs. Brown walitokea kumpenda sana binti yao  Jenifer kwani ndio mtoto pekee wa kike hivyo walionesha upendo mwingi  kwa binti yao kwa kumtimizia mahitaj yote muhimu na kumpa kila  alichokitaka binti yao ili wamridhishe na kuhakikisha wanampa malezi  bora na kujenga upendo imara kwa binti yao. Kutokana na hali ya  ngumu  ya maisha iliyokuwepo katika familia hiyo ya Mr. Brown na Mrs. Brown,  wazazi hawa walikaa na kujadili njia sahihi ya kuweza kukabiliana na  umasikini walio nao na kuweza kujikwamua kimaisha wakapata wazo la  kumpeleka shule binti yao Jenifer ili hapo baadae aje kuwasaidia wazazi  wake kupitia elimu atakayoipata shule hivyo wazazi wakakubaliana na  kuanza mipango ya kumuandikisha shule binti yao ili aanze kusoma, wazazi  wa Jenifer walijitahidi kutafuta pesa kwa hali na mali ikapelekea  wazazi wa Jenifer kujiunga na kampuni zinazotoa mikopo ya fedha lengo  kupata pesa waweze kumtimizia mahitaji binti yao aweze kuanza shule.  Mungu alileta kheri kwa wazazi hao na kufanikisha kuipata pesa ya  kumpatia binti yao kwa ajili ya matumizi madogo madogo ya shule na binti  yao akafanikiwa kuanza elimu ya msingi akasoma darasa la kwanza mpaka  darasa la saba lakini alipo maliza darasa la saba matokeo yake hayakua  mazuri hivyo hakuweza kuchaguliwa katika shule za serekali kwa ajili ya  kuendelea na elimu ya sekondari lakini wazazi wa Jenifer hawakukata  tamaa na waliendelea kuwa na moyo wa kumsaidia binti yao Jenifer kwa  vyovyote vile mpaka waone mwisho wake kwani malengo yao binti yao asome  mpaka daraja la juu afike mpaka chuo kikuu, baada ya Jenifer kumaliza  elimu ya msingi na hakufanikiwa kufanya vizuri katika mitihani yake  ikabidi wazazi wajipange upya kutafuta ada ya kumlipia binti yao ili  aweze kujiunga na elimu ya sekondari kwa dhumuni la kuhakikisha binti  yao Jenifer anaendelea na elimu. Mungu hakuitupa familia hii ya Mr na  Mrs. Brown aliwajaalia wakafanikiwa kuipata pesa ya kumlipia ada binti  yao na wakamuandikisha katika shule ya kulipia ya sekondari  iliyofahamika kwa jina la  "GARDEN SECONDARY SCHOOL" Jenifer alijiunga na shule  hii na kuanza elimu yake ya sekondari lakini kama ilivyo kwa vijana  wengi wa kisasa kutofahamu umuhimu wa elimu na kushindwa kujua nini  wanapaswa kukifanya pindi wanapo kuwa shule ndivyo ilivyokuwa kwa  Jenifer. Jenifer hakujua umuhimu wa elimu na hakuona juhudi za wazazi  wake kwake za kutafuta pesa kwa ajili ya kumlipia ada ili aje kuwasaidia  baadae na kuwasaidia wadogo zake Peter na Joseph. Kipindi Jenifer  alipokua shuleni hapo akiendelea na elimu ya sekondari tabia yake  ilibadilika akawa anautumia muda wake mwingi wa shule kujichanganya na  marafiki ambao hawakuwa na msaada mzuri kwake na wakati mwingine alikua  akiaga kwao anakwenda shule lakini alikua hafiki shule alikua anakwenda  kwa marafiki anashinda na kurudi nyumbani wazazi wake hawakujua  kinachoendelea kwa binti yao. Wakati mwingine Jenifer alikuwa ni mtu wa  kupenda sana kwenda kwenye kumbi mbali mbali za starehe wakati alikua  anatoka nyumbani kwao usiku akiwaaga wazazi wake kuwa anakwenda kwa  marafiki zake anaosoma nao wanakwenda kukesha wakisoma na kujadiliana  yale waliyofundishwa shuleni, wazazi wa Jenifer hawakuwa na kipingamizi  kwa binti yao walikua ridhwaa kukubaliana na kila anachohitaji binti yao  ili mradi kumridhisha na kumfanya awe huru ili mwisho wa siku aweze  kutimiza ndoto za wazazi wake hivyo wazazi walikua wakimpa ruhusa binti  yao atoke usiku wakidhani anaenda kusoma na wenzake kumbe Jenifer alikua  anatumia muda huo kutoka na kwenda CLUB (kumbi za starehe) na marafiki  zake wanaenda kujirushana alikua anarudi nyumbani kwao kesho yake asubuhi,  na ilikua kila ikifika siku ya Ijumaa mosi ndio anatoka usiku na  wenzake, siku moja kama kawaida yake Jenifer na wenzake wametoka na  kwenda kwenye kumbi za starehe huku nyumbani wazazi wanajua watoto wao  wameenda katika masomo yao kama ilivyozoeleka, kipindi wapo CLUB kuna  mwalimu wao wa shule alikuwepo katika ukumbi huo wa starehe na akakutana  na kundi hili la wakina dada kama wanne akiwemo na Jenifer wakiwa  wamevaa mavazi mafupi ya ajabu kama machangudoa wanaojiuza, yule mwalimu  wao alichokifanya akawaita kisha akawaambia "NAOMBA SIKU YA IJUMAA TATU  MKIFIKA SHULE CHA KWANZA NAOMBA NIWAKUTE OFISINI KWANGU KAMA MLIVYO  WANNE TENA MJE MKIWA MMEVAA HIZI NGUO MLIZO ZIVAA NA KILA MMOJA WENU AJE  NA MZAZI WAKE" kisha mwalimu akawaambia wawe huru waendelee na mambo  yao ila ikifika siku ya Ijumaa tatu siku ya shule wafanye kama alivyo  agiza mwalimu huyo pale pale Jenifer na wenzake wakakosa amani na mudi  ya kuendelea kufurahi usiku ule ikatoweka na kila mmoja wao akawa  anawaza itakuaje hiyo siku ya Ijumaa tatu na wataanzia wapi kuwaeleza  wazazi wao juu ya kosa hili walilofanya mpaka wamekutana na mwalimu  kawaomba waende shule na wazazi wao.....?!