Sikuamini nilivyokua nasikia maneno ya watu mtaani kuhusu mke wangu maana nilimpenda sana na tuna mtoto mmoja hivyo niliona wanataka kutugombanisha tu.
Mimi ni mfanyabiashara, na mara nyingi hua nasafiri kwenda mikoani kufanya kazi zangu na kurudi.
Mwanzoni niliishi vizuri na mke wangu wala hakukua na tatizo, ila jinsi muda ulivyokua ukienda ndivyo mke wangu alikua akibadilika.
Nikiwa mkoani, nilimuacha ndugu yangu wa kiume nyumbani kwangu akae na shemeji yake na mtoto.
Nikiwa huko majirani walikua wakinipigia simu na kuniambia tabia za mke wangu na jinsi anavyotoka na wanaume ovyo pale mtaani, niliumia sana, lakini kila nikimuuliza yule ndugu yangu hakuweza niambia ukweli nafikiri alikua anaogopa kutugombanisha.
Nikirudi nyumbani ni ugomvi tu usioisha na mke anaishia kwenda bar na kunywa pombe na kurudi usiku sana, na kutotimiza wajibubwake kama mke.
Kuna kipindi inaweza pita hata mwaka mke hanipi unyumba, lakini nikiwa mkoa nasikia anatoka na wanaume wengine.
Nikirudi ni ugomvi na hua nashikwa na hasira kutaka kumpiga sana hata kumtoa uhai, lakini nikimfikiria mtoto wetu hua nakua mpole na kumsihi aache ujinga na umalaya. Mke hua ananiahidi kua atabadirika lakini siku mbili nyingi ataanza tena kulewa na kutembea na wanaume za watu.
Kuna kipindi tulikua tunatafuta mtoto wa pili, lakini kila nikifanya mahesabu yangu ya uhakika kupata mtoto, mke wangu hashiki. Kila nikimmwagia kipindi nyeti kile ashiki. Kumbe masikini ya mungu alikua akitoa zile mimba bila huruma.
Nilihisi swala hilo maana kuna siku nilimmwagia siku danger na alishika mimba lakini siku moja alilalamika maumivu ya tumbo sana na wakati haikua muda wake wa period. Kitendo kile kiliniumiza na kujikuta nikianza kutafuta katoto kengine nje.
Na nilifanikiwa kumpata mtu mwingine nje na kuzaa nae mtoto, lakini nilijishtukia na kujikuta nikimwambia mke wangu kuhusu swala hilo..
Daah ilikua kosa sana kumwambia swala hilo maana ndo alizidisha na akawa halali kabisa ndani siku zingine.
Nilipeleleza ni nani anatoka nae mke wangu, na niligundua mtu anayetoka na mke wangu, ni muhuni tu wa mtaani asiyekua na dira ya maisha kabisa.
Nilishauriana na watu wa karibu kwangu tufanyeje kuhusu mke wangu, na wao walinipa ushauri wa kwenda kwa wazazi wake na kukaa nao kitaa ili wamuonye binti yao.
Tulienda kwa wazazi wake huyu mke na yeye alikuwepo. Uzuri ni kwamba hadi baba mkwe alishasikia tabia zake kutoka kwa jirani yao.
Wakati wa mashauriano pale, binti aliinuka katikati ya mazungumzo na kututukana wote na kuondoka zake…
Baba mkwe aliumia sana kwa kotendo kile na kuniambia kua niamue chochote nachoweza fanya maana tabia ya binti imejidhihirisha kua hataki suluhu au kurudi…
Nilishangazwa sana na tabia ya mke wangu ilivyofikia, sikujua kama amerogwa au laah. Daaah maisha haya, ee mungu nimekosea wapi mimi…
Itaendelea….