TAFUTA HAPA

Baada Ya Kumaliza Masomo – Sehemu Ya Kwanza

Ni story ya binti mmoja aitwaye Caroline na mwenzake anaitwa Anna na maisha yao baada ya kumaliza elimu ya chuo na kuanza kula bata kupoteza stress za kitabu kwanza.
“Oooh finally nimemaliza mitihani” alisema Anna huku akitoka kwenye chumba cha mtihani na kujihisi akiwa huru kabisa na kuelekea hostel kwa rafiki yake Caroline.
Alifurahi sana siku hiyo na kutaka kurefresh sana ili atoe stress zoote za kitabu, caroline akamkaribisha na kumwambia “bora umefika, umetumia muda mrefu kwenye mtihani”, huku akitabasamu.
Anna alifurahi na kuuliza bata wapi siku hiyo maana alitaka ule usiku uwe usiku wake na uwe wa kuukumbuka maishani mwake.
Huku wakijadiliana , caroline akasema “sasa ili leo usiku wako uwe mzuri inabidi kumkamata yule handsome wa chuo yule, nae leo atatoka out kula bata na maeneo si tunayajua, alafu hua anakukubali sana yule”. Huku anna akitabasamu na kurembua ni dhahili nae alikua akifikria hivyo.

“Sasa nimekuandalia mtoko wa maana wa kumfanya mwanaume yeyote akuangalie mara mbili”.. Mhh anna aliguna na kucheki huo mtoko ulioandaliwa na rafiki yake.
Ilikua ni gauni fupi sana jekundu lenye kubana sehemu za kiuno na kuonyesha mapaja, anna alifurahi na wote wakajiandaa na kuvaa hivyo usiku huo, kisha wakaenda kula bata.
“sasa leo anna inabidi ujiachie na umchukue mwanaume mmoja akakupooze usiku kucha yaani uwe usiku mtamu wa leo” alisema caroline huku akimuangalia anna wakiwa kwenye nyumba iliyokua inafanyika party kwenye high table..
“leo lazima, tufurahi wote”, anna alisisitiza. Huku akicheza cheza mwenyewe kwenye kiti kirefu na mapaja yake kuonekana sana yakiwa meupeeee.
“umeona mtoto unavyoringa mwenyewe, sasa nenda kacheze pale kati, si unajua jinsi ya kumkamata mwanaume, kacheze na ufurahi” caroline alimwambia anna.
Anna alitoka kwenye kiti akaenda sehemu watu walipokua wakicheza, nae akaanza kucheza huku akiipandisha na kuishusha gauni lake fupi. Ghafla akasikia mikono miwili ikimkumbatia kiuno chake huku jamaa akimbambia na kumnong’oneza masikioni “aaah uu mzuri sana na unacheza vizuri sana, si vizuri nikaumia nafsi kukuangalia ukiwa unacheza mwenyewe tu”…
Anna alitabasamu na kuendelea kumdatisha yule mwanaume kwa kumkatikia vizuri na kumchezea kwa mahaba, anna alifurahi sana na baadae akamgeukia kumuangalia, aaah kumbe ndo yule handsome aliyekua anamzungumzia na caroline. Basi hapo anna ndo mizuka akaibandisha zaidi na kujiachia zaidi.
Huyo mkaka anaitwa sebastian. Walicheza pamoja na kunywa na kupiga story sana mpaka ilipofikia mida ya saa sita. Sebastian akamvuta anna na kwenda nae korido na kupiga nae romance, kisha anna akamtext caroline “nipo na yule handsome tuliyemzungumzia, naondoka nae, si sawa tu?”..
Caroline alijibu fasta “hee uko fasta, unauhakika unataka kwenda nae?”, anna akamjibu “eeh si usiku wa kuumbuka remember tulivyokubaliana..”. Basi caroline akatabasamu “haha go girl nenda kafurahi…”.
Anna aliingia ndani na sebastian kwenye nyumba ya sebastian na kuufanya usiku uwe mnono, usiku huo anna alipigwa mambo mara tano, yaani akilala kidogo tu sebastian anamuamsha na kuanza vitu, usiku ulikua mzito sana na anna alifurahi sana..
Asubuhi yake anna aliwahi kuamka na kuoga fasta na kuondoka huku akiacha kiujumbe “hakika usiku ulikua mtamu sana, nitaukumbuka, ila hautarudia” huku akichukua namba ya sebastian kwenye card yake na kuondoka.
****************
Baada ya miezi mitatu nikiwa nipo sehemu yangu na nimepata kazi tayari, nilianza kuumwaumwa na kubagua vyakula sana, kisha nikamtumia mesage caroline na kumuuliza shida inaweza kua nini, na baada ya nusu saa nikajikuta nipo chooni nikicheki kipimo cha mimba…
“dah, mungu wangu, heee au kimekosea, nina mimba!!, yaani ule usiku heee”. Alijikuta akiwaza usiku ule na sebastian ulivyokua na kuangalia kipimo cha mimba alichokishika mkononi chooni…
Machozi yalianza kumtoka anna huku akiwaza sana alichokifanya siku ile na huku akikiangalia kile kipimo. Alijikuta hajui afanye nini na ni kwa mara ya kwanza anajisikia hivyo.. Alikua na plan nyingi za kujiendeleza kimasomo zaidi na kimaisha kwakua baba yake alishafariki na mama yake anamuangalia sana yeye ili aje kumsaidia. Anna alionekana kuchanganyikiwa sana.
“ni lazima nimwambie sebastian kuhusu hili, najua atanikumbuka tu maana usiku ule alilala na mimi tu mpaka asubuhi, lazima atanikumbuka”, aliamka chooni na kujipa moyo kua kuna kiumbe kinakua ndani yake na kinahitaji upendo, matunzo na baba pembeni.
Alienda kitandani na kujilaza akiangalia juu na kujisikia kizunguzungu kiasi, kisha akampigia rafiki yake caroline na kumwambia kua ana mimba na kwamba ana uhakika itakua ya sebastian tu maana hakua na mwanaume mwingine. Caroline alisisitiza kua ni ya sebastian maana tangu wapo chuo anna hakuwahi kua na boyfriend zaidi ya usiku ule aliolala na sebastian.
Anna akamuomba caroline amsaidie kupata namba ya sebastian kwakua alikua anajuana na marafiki wengi wa sebastian. Baada ya dakika kama kumi, caroline akamtumia namba ya sebastian.
Anna alivuta pumzi kabla ya kumpigia sebastian, kisha akampigia, na baada ya kuita mara tano, sebastian alipokea na ikawa hivi:
Seb: “hallow, nani mwenzangu”
Anna: “eerm, hi sebastian, ni anna naongea”
Seb: “unahitaji nini kutoka kwangu?”
(Alionekana mwenye hasira sijui kafanywa nini.)
Anna: “usijifanye una hasira, unajua tulikutana kimwili miezi kadhaa iliyopita…”
Seb: “yani zile round tano za ule usiku hazikukutosha, unataka zingine au? Maana asubuhi ukanikimbia, mbona ulikua unaonekana msichana mpole na usiyeweza kuhimili mambo makubwa, achana na mimi na hatuta lala tena usiku kama vile sawa”.
Anna: “sebastian ninachotaka kukwambia ni cha muhimu”
Seb: “hamna utakachoniambia kitakachobadili mawazo yangu”
Anna: “unajua nina” … Akahema kwanza… “mimba”..
Simu ilikatwa kabla sijamalizia neno mimba, na nauhakika hakunisikia vizuri kua nina mimba yake, anna alijaribu kupiga simu tena na tena kama mara tano lakini haikupokelewa.
Siku kadhaa mbele anna aliweza kuongea nae na kupanga siku akutane nae waongee vizuri, kwakua muda mwingi alikua busy na kusimamia kampuni yao ya kifamilia. Wakati anaongea nae kwenye simu, anna alisikia kuna mwanamke akiongea pembeni ya sebastian na kumpora simu aliyokua akiongea kisha yule mwanamke akamwambia sebastian akaendelee na kazi alafu akapokea simu ile kuanza kuongea na anna na kumwambia
“wewe najua umesoma na sebastian na amenielezea kua ni mmoja ya wale wasichana wanotaka kulala nae tu kitandani na kwenda zao, kama ulikua hujui, mimi ni mama yake wa kambo, na sebastian yupo busy sana, hivyo acha kumsumbua sawa… Na eti umelala nae usiku mmoja alafu unaomba upate mimba mimba kisa huyu ni tajiri, acha kuota sawa, kawapelekee wanaume wengine uliolala nao sawa”
Anna akajibu “sidanganyi, mtoto ni wake sebastian..”
Yule mama wa kambo alicheka sana na kumwambia “tumia akili wewe malaya, yani alale na wewe usiku mmoja na hamjawahi kua hata na mahusiano tena mizei mitatu imepita alafu uje kusema una mimba yake”
Anna kwa hasira akakata simu na kumpigia caroline na kumuelezea kilichotokea, caroline alimuita kwake wakaongee na kumliwaza..
Anna alikua akilia muda mwingi, caroline alimshangaa na kumwambia “hee sijawahi kukuona ukilia hivi, embu punguza bana, mambo yatakaa sawa tu” “mimi nitakusaidia kwa kila kitu wala usiwe na wasiwasi, huyo sebastian tutamvaa tu siku we subiri, na hiko kimama chake cha kambo tutakinyoosha vile vile”
Nini kitatokea, Usikose sehemu ya Pili…..